• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU

Posted on: December 15th, 2024

Makamu Mwenyekiti tume huru ya Taifa ya uchaguzi, Jaji (R) (MST) Mbarouk S. Mbarouk amesema kuwa watu wenye mahitaji maalumu watapewa kipaumbele cha kujiandikisha bila ya kulazimika kusubiri kupanga foleni.

Mhe. Mbarouk ameyasema hayo  Disemba 15, 2024 Wakati akifungua  mkutano wa tume na Wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa uliyopo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wenye kauli mbiu ya inayosema "Kujiandikishia kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora".

Akizungumza katika ufunguzi huo Mhe. Mbarouk amefafanua kwamba hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa haki za watu wenye ulemavu, wazee, na makundi mengine yenye mahitaji maalumu zinaheshimiwa na kutekelezwa kwa usawa hivyo  mchakato wa kujiandikisha katika daftari la kudumu utaendelea kuwa rahisi kwa watu hao ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi bila vikwazo vya aina yoyote.

"Ni muhimu kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi bila kujali changamoto anazokutana nazo, Kwa hiyo watu wenye mahitaji maalumu watapewa kipaumbele maalumu katika vituo vya kujiandikisha ili wasiwekewe vikwazo vya aina yoyote na hakuna mtu atakayezuiliwa kutokana na hali yake ya kiafya au kimwili", amesema Mbarouk


Pia ameongeza kwa kusema  kuwa Tume ya Uchaguzi itahakikisha kuwa vituo vya kujiandikisha vitakuwa na mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa vifaa na msaada wa ziada ili kuwasaidia katika mchakato huo na kuongeza kwa kutoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano na kuhamasisha watu wenye mahitaji maalumu kujitokeza na kujiandikisha ili waweze kutumia haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi ujao.


Mkutano huo uliofanyika Mkoani Iringa ni sehemu ya jitihada za Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuelimisha na kuwashirikisha wadau wa uchaguzi kuhusu umuhimu wa kujiandikisha kama wapiga kura na umuhimu wa kuwa na daftari la mpiga kura.

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.