• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

WATUMISHI WA MAHAKAMA MSITOE WALA KUPOKEA RUSHWA - RC SERUKAMBA

Posted on: February 3rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewasisitiza Watumishi wa mahakama nchini kuwa waadilifu na kuepuka rushwa kwani ni kikwazo katika kujenga Taifa bora.Ameyasema hayo  Februari 03, 2025 wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mahakama Kuu ya Tanzania Mkoani Iringa.Mhe. Serukamba amesema kuwa wanasheria wanapaswa kupambana na Rushwa kwani ni Adui wa haki kwa kuwa watu wengi wanakosa haki zao kwa Sababu ya Rushwa.Aidha Mhe. Serukamba ameongeza kuwa wanapoongelea Dira ya 2050 wanapaswa kujenga jamii iliyo bora yenye haki,usawa na wasitoe wala kupokea rushwa ili pawepo na taifa lenye maendeleo.Pia Mhe. Serukamba ameeleza na kuomba kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa na elimu ya sheria ili kuepuka migogoro na kufanya jamii kuwa na amani na utulivu ili kuwa na Taifa endelevu na lenye maendeleo katika nyanja tofauti tofauti.Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Iringa, Dunstan Ndunguru wakati akisoma taarifa inayohusu maadhimisho hayo amefafanua kwamba mahakama katika kipindi cha wiki hiyo imefanikiwa kufanya maonyesho ya huduma zinazotolewa na mfumo wa haki za kisheria na namna wananchi wanavyoweza kutumia huduma hizo ili kulinda haki zao. Akiendelea kuzungumzia maadhimisho hayo Ndunguru amesema kuwa maonyesho hayo yalijumuisha utoaji wa elimu kuhusu sheria za familia, urithi, kazi, na haki za watoto, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuwaelimisha kuhusu masuala ya kisheria.Ikumbukwe kuwa  maadhimisho hayo ya wiki ya sheria yalianza mkoani Iringa Januari 25 mpaka Februari mosi mwaka huu na kilele chake kikiwa ni leo Februari 03, 2025 huku Kauli mbiu  ikiwa ni "Tanzania 2050 Nafasi ya Taasisi zinazosimamia Haki, Madai katika kufikia Malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo".

Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.