• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Iringa Region

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Iringa Region

  • Home
  • About Us
    • History
    • Location
    • Vision and Mission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Administration
    • Organisation Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Education
      • Planning and Coordination
      • Health and Social Welfare
      • Economic and Production
      • Infrastructure
      • Water Service
      • LGAs Management
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Service
      • Procurement Management Unit
  • Districts
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • District
    • Iringa MC
    • Mafinga TC
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Investiment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Ruaha National Park
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
    • Civil Servant Cervices
  • Publications
    • Guidlines
    • Policies
    • News
    • Forms
  • Media Center
    • Photo Gallery
    • Videos
    • News Later
    • Events

ZAIDI YA 30% YA MAVUNO HUPOTEA SHAMBANI

Posted on: June 25th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Wakulima nchini wamekuwa wakipoteza zaidi ya asilimia 30 ya mavuno na kuwanyima wakulima kunufaika na jasho lao.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake kwenye zoezi la uhamasishaji wa kupunguza upotevu na uharibifu wa zao la mpunga pamoja na kuhifadhi pamoja ili kuwa na soko la uhakika katika tarafa ya pawaga, wilayani Iringa.

Masenza alisema kuwa uhifadhi na utunzaji duni wa mazao umekuwa ukisababisha upotevu wa mavuno jambo linaloathiri kipato cha mkulima. “Takwimu zinaonesha kuwa upotevu ni takribani asilimia 30- 40 ya mavuno yote ya mkulima na hutokea baada ya mavuno. Hiki ni kiwango kikubwa sana ambacho kinawanyima wakulima uwezo wa kufaidika kutokana na jasho lao lakini pia kinaipa Wilaya, Mkoa na Nchi changamoto kubwa ya kuhakikisha uhakika endelevu wa chakula hapa nchini’ alisema masenza. Kwa kiasi kikubwa upotevu husababishwa na ukaushaji usioridhisha, mbinu duni za uvunaji, shambulio la wadudu na visumbufu” alisema Masenza.  

Akiongelea uhifadhi wa mazao kwa pamoja ghalani, mkuu wa mkoa alisema kuwa serikali imekuwa ikichukua hatua kwa kushirikiana na wadau kukabiliana na tatizo la upotevu na uharibifu wa mazao. Hatua hizo alizitaja kuwa ni  kuelimisha wakulima jinsi ya kudhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvunwa, njia bora za uhifadhi pamoja na kujenga maghala bora. Kujenga maghala ya kuhifadhia mazao peke yake hakutoshi kudhibiti uharibifu huo. Uharibifu na upotevu wa mavuno hutokea tangu hatua ya kuvuna hadi kuandaliwa kuliwa, aliongeza.

“Serikali kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) wametenga fedha kwa ajili ya mradi wa kupunguza upotevu wa mpunga kabla na baada ya mavuno na kuongeza mnyororo wa thamani na soko la mchele kwa wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa” alisema Masenza.

Wakati huohuo, mkuu wa mkoa aliwaagiza viongozi wote wa vijiji, Kata na Tarafa wakiwepo Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Madiwani na Maafisa Tarafa wawe mfano wa kuanza kuhifadhi ghalani na kumpatia tarifa ya utekelezaji. Vilevile, Viongozi wafanye mikutano ya uhamasishaji kwa wakulima kila kijiji na sehemu ya kuuzia mpunga/mchele iwe ni katika maghala yaliyojengwa ili kuzuia wakulima wasindelee kupunjwa na wafanyabiashara kwa kuwapa bei ndogo.  

=30=


Announcements

  • No records found
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • View All

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
More Videos

Quick Links

  • Iringa Region Revenue Collection
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Related Links

  • State House
  • Public Service Recruitment Secretariat
  • PORALG
  • National Bureau of Statitics
  • Information Department
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

COUNTER-free

Map

Contact Us

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Telephone: +255 262 702 715

    Mobile:

    Email: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.