• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

BENKI YA MUCOBA KUTOA MIKOPO STAKABADHI GHALANI

Posted on: June 25th, 2018

Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Benki ya MUCOBA kutoa fursa ya mikopo ya stakabadhi ghalani ili kuwanufaisha wakulima wa mpunga wilayani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya uzinduzi wa mfumo wa mikopo ya stakabadhi ghalani kupitia benki ya MUCOBA katika Tarafa ya Pawaga, wilayani Iringa.

Masenza alisema kuwa wakulima wamekuwa na changamoto ya upatikanaji bei nzuri ya mpunga katika Tarafa ya Pawaga. “Jambo hili limesababisha wakulima wetu kuendelea kunyonywa na walanguzi kwa kuuza mazao yao kwa bei ya chini na kusababisha wakulima wa Mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuendelea kuwa masikini na huku walanguzi wakiendelea kuneemeka zaidi kwa jasho la wakulima wetu. Hivyo basi, kwa uamuzi huu wa Benki ya MUCOBA wa kuweza kuanzisha fursa hii ya mikopo ya stakabadhi ghalani ili wakulima wetu waweze kutunza mazao yao katika Ghala hili na kupewa mikopo ya riba nafuu, ili kusaidia wakulima kujikimu wakati wakisubiria soko na bei nzuri za mazao yao” alisema Masenza. Benki ya MUCOBA ni ukombozi kwa wakulima wa mpunga katika Tarafa ya Pawaga, alisema. Aidha, aliwataka wakulima wa mpunga wa Pawaga kuchangamkia fursa hiyo muhimu na kuunga mkono juhudi za benki na serikali.

Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa wadau kushirikiana na benki ya MUCOBA kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kutumia fursa ya mikopo ya stakabadhi ghalani. “Ninatambua ukweli kuwa wakulima wengi hawana elimu ya  kutosha kuhusu stakabadhi ghalani, hivyo napenda kutoa wito kwa wadau wengine wote  kushirikiana na Benki ya MUCOBA  kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kutumia fursa hii ya mikopo ya  stakabadhi ghalani  na pia kutumia huduma bora za benki ya MUCOBA hapa Pawaga na maeneo mengineyo ambako Benki inafanya shughuli zake. Pia sisi kama serikali tutakuwa bega kwa bega katika kusaidia juhudi za kuwaelimisha wakulima wetu juu ya umuhimu wa stakabadhi ghalani, pia hatuta sita kusaidiana na Benki yetu ya wananchi MUCOBA kupeleka huduma hii mahali pengine” alisema Masenza.  

Benki ya MUCOBA imefungua kituo cha huduma za kifedha katika Tarafa ya Pawaga ili kuweza kuwahudumia wananchi wanyonge kupata mikopo kwa ajili ya kilimo cha mpunga wilayani Iringa.

=30=


Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ‎RC SERUKAMBA AITAKA TRA KUDHIBITI RISITI FEKI, KUHAMASISHA ELIMU YA KODI

    May 19, 2025
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM MKOA WA IRINGA.

    May 18, 2025
  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.