Sehemu/Idara hii ina lengo la kusaidia au kuwezesha utoaji huduma za uendelezaji wa Elimu ikijumuisha usimamizi wa elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya watu wazima na inayotolewa katika njia isiyo rasmi; na mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Sehemu/Idara hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni Afisa Elimu wa Mkoa ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Sehemu/Idara ya Huduma za Elimu
•Kuratibu uongozi wa shule za awali, Msingi, Sekondari, elimu ya watu wazima na Elimu rasmi
•Kuratibu ajira na usambazaji wa walimu wa shule za awali, msingi na sekondari katika Mkoa
•Kuratibu utekelezaji wa sera za Elimu na mafunzo ya ufundi ndani ya Mkoa na kutoa Ushauri kadiri inavyohitajika.
•Kusimamia mitihani ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu katika Mkoa.
•Kuratibu ukusanyaji, tathimini, uunganishaji/uandaaji, kutafsiri na kutoa taarifa/takwimu za elimu na mafunzo ya ufundi katika Mkoa
•Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa taarifa za ukaguzi
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya utekelezaji wa sera ya utamaduni na michezo
•Kuratibu shughuli zinazohusiana na michezo katika Mkoa na kuendesha mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA Mkoani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.