Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Mashaka Mfaume, kutenga Kiasi cha Shilingi Millioni 12 ili kukamilisha miundombinu ya shule mpya ya Sekondari iliyopo Kijiji cha Kinengembasi.
Maagizo hayo ameyatoa leo 08,Mei,2025 wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
Akiwa katika shule baada ya kukagua na kujionea ujenzi wa shule hiyo ambayo baadhi ya maeneo hayajakamilika na kukamilika kwake kunahitaji shilingi Millioni 12, Mhe. Serukamba amemuagiza Mkurugenzi kutoa kiasi hicho ili kukamilisha miundombinu ya shule hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.