• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

IRINGA KUENDELEZA MAZAO YA BIASHARA

Posted on: May 14th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Mkoa wa Iringa unaendelea kuweka mikakati ya kuendeleza mazao ya korosho, pamba na kahawai ili yachangie katika kukuza uchumi wa wakulima na mkoa kwa ujumla.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua jukwaa la ushirika mkoa wa Iringa kililofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo hivi karibuni.

Masenza alisema kuwa serikali inatambua mazao matano ya kimkakati na kuyataja kuwa ni korosho, kahawa, tumbaku, pamba na chai. “Mkoa wetu wa Iringa una hali ya hewa nzuri inayofaa kwa kilimo cha mazao yote. Kumekuwa na maendeleo mazuri katika kilimo cha chai ambapo uzalishaji umefikia kiasi cha tani 18,930 kwa mwaka 2016/2017, kwa mazao ya korosho, pamba na kahawa mkoa wetu unaendelea kuweka mikakati thabiti wa kuyaendeleza” alisema Masenza.

Halmashauri zimeanza kuweka jitihada za kuhamasisha kulima mazao hayo alisema. “Kupitia jukwaa hili nawaagiza wakurugenzi wa halmashauri kukaa chini na vyama vya ushirika kuandaa mpango wa miaka mitano wa kuendeleza mazao hayo” aliagiza Masenza.

Alisema kuwa wananchi wakihamasishwa kuzalisha mazao hayo kwa wingi, kutawaongezea wanaushirika kushiriki shughuli za uzalishaji mazao ya kibiashara na kuongeza kipato cha wanaushirika na wananchi kwa ujumla.

Akiongelea zao la tumbaku, mkuu wa mkoa alisema kuwa mkoa wa Iringa umekuwa ukizalisha tumbaku kwa zaidi ya miaka 50 lakini zao hili halijatoa mchango mkubwa kiuchumi kwa wananchi. “Napenda kutoa rai kuwa tunatakiwa kujipanga upya ili kuendeleza uzalishaji wa zao hili. Uzalishaji wa zao la tumbaku umekumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa soko na uwepo wa madeni makubwa katika vyama vya msingi ambayo yanasababishwa na wanachama kutouza kupitia vyama vyao. Nachukua fursa hii kuwaasa wakulima wa zao hili kuzingatia taratibu za kilimo hicho hasa kutowatumia watoto, kupanda miti na kuuza kwa uaminifu kupitia vyama vya ushirika” alisisitiza Masenza.

Jukwaa la ushirika ni jukwaa la pili kufanyika ngazi ya mkoa, likishirikisha Katibu Tawala Mkoa, wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa, wadau wa taasisi za kifedha na wanaushirika.

=30=

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.