Na. Dennis Gondwe, Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- IRINGA
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi ametoa vifaa vya michezo kwa shule ya sekondari ya ufundi Ifunda ili kuhamasisha michezo na nidhamu shuleni hapo.
Mhe Hapi alitoa ahadi ya kuinunulia vifaa vya michezo shule hiyo alipokuwa akiongea na jumuiya ya shule hiyo iliyokutanisha pamoja walimu, wanafunzi na wafanyakazi baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya shule hizo uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.
Mhe Hapi ambaye alikuwa kaka mkuu katika shule ya ufundi ya wavulana Bwiru katika kipindi chake aliwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo kudumisha nidhamu na kuchapa kazi. “shukrani ya pekee mnayoweza kutoa kwa serikali ni matokeo mazuri katika masomo yenu.
Vifaa alivyochangia ni mipira (5) ya basketi, mipira (5) ya soka, mipira (5) netiboli, mipira (3) voliboli, neti (2) kwa ajili ya mpira wa soka na neti (1) kwa ajili ya voliboli. Vilevile, aliahidi shilingi 500,000 kwa ajili ya klabu ya “debate”.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa akiwa katika shule ya sekondari ya wasichana ya Ifunda aliahidi mipira (5) ya netiboli na kukabidhi shilingi 100,000 kwa kwaya ya shule hiyo.
Ikumbukwe kuwa Mkuu wa Mkoa yupo katika siku yake ya pili ya ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa wilayani Iringa katika Tarafa ya Kiponzelo.
=30=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.