Majukumu ya Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa ni pamoja na;
i. Kuzishauri na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziwezekuwa na matumizi sahihi ya fedha za Umma,
ii. Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kuimarisha Utawala Bora,
iii. Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kufanya mapitio ya miundo na mifumo kwa ajili ya kuimarisha utendaji,
iv. Kufanya ukaguzi wa kila robo mwaka na ule wa kushtukiza kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa,
v. Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maandalizi na utekelezaji wa Bajeti,
vi. Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika usimamizi wa rasilimali watu,
vii. Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi,
viii. Kuratibu maandalizi na kufanya ufuatiliaji na tathmini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa,
ix. Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya utekelezaji wa Sheria za kazi,
x. Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika maandalizi ya Sheria ndogo za Mamlaka za Serikali za Mitaa na masuala ya Ukaguzi wa ndani,
xi. Kuratibu uhamisho wa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (Uhamisho wa ndani na nje ya Mkoa).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.