Sehemu hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Sehemu ya Miundombinu:
•Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Viwango katika nyanja za Barabara, Majengo, Nishati, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika nyanja za Barabara, Majengo, Nishati, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
•Kuwasiliana/kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala ya Ujenzi
•Kushauri juu ya Masuala ya barabara, Nishati, Ujenzi, Viwanja na uboreshaji mifumo
•Kusimamia na kushauri juu ya kazi za Ujenzi zinazotekelezwa ndani ya Mkoa
•Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutwaa ardhi kwa ajili ya matumizi ya Serikali Kuu
•Kuandaa ramani kwa ajili ya mipangomiji
•Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya Tathimini ya Athari za Kimazingira
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza maeneo ya wanyamaporI
Sehemu hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulika na Miundombinu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.