Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amehimiza Wazazi na Walezi Nchini kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu na kuwahimiza watoto hao juu ya Umuhimu wa Elimu kwani Elimu ndio Nguzo ya maendeleo ya jamii na UchumiAmeyasema hayo leo Septemba 20,2024 wakati akihutubia kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule ya Real Hope iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi.Mhe Serukamba Amesema kuwa jambo kubwa ambalo watoto wanatakiwa kurithi kutoka kwa wazazo wao ni Elimu hivyo wazazi wametakiwa kulipa kipaumbele suala la elimu ili kuleta maendeleo katika jamiiAidha Mhe. Serukamba ameongeza kwa kuwataka wasomi wote kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwa kusoma vitabu mbalimbali kwani kwa sasa sayansi na Teknolojia ikekuwa kwa kasi tofauti na hapo awali.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameagiza kumfuta kazi fundi anayejenga madarasa katika shule ya Sekondari ya wasichana Lugalo na shule ya Ikokoto kwa kutokamilisha miradi kwa wakati huku akimuagiza afisa manunuzi kumwondoa mmoja wa wazabuni kwa kuchelewesha vifaa vya ujenzi kwenye miradi ya Halmashauri ya Wilaya Kilolo.Hayo yamejiri leo septemba 19,2024 wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa shule ambapo awali alianza kukagua katika shule ya sekondari ya Ifingo ambapo alikuta mradi bado haujakamilika na vifaa bado havijafika katika eneo hilo na baadae alifika katika shule ya Sekondari Kilolo ambapo huko alikutana na tatizo la kutokuwepo kwa vifaa vya ujenzi lakini alipofika katika Shule ya Wasichana ya Lugalo napo huko akakutana na kisa kingine ambapo fundi Ndg.Godwin Mshana aliyepewa kazi ya ukamilishaji wa madarasa kasi ya utendaji kazi yake kusuasua ambapo Mhe.Serukamba amemwagiza Mkurugenzi Tarehe 26 mwezi huu kama atakuwa hajafikisha majengo kwenye lenta basi afutwe kazi apewe kazi mtu mwingine huku akimfuta kazi fundi huyo kutoendelea na ujenzi katika shule ya IkokotoPia Mhe Serukamba ameagiza kumondoa Mzalendo ambaye ni mmoja wa wazabuni kwa kushuindwa kupeleka vifaa kwa wakati na kupelekea ujenzi kusuasua na kuagiza kumuweka mzabuni mwingine ambaye ni CF.sambamba na hayo Mhe. Serukamba ameendelea kuwahimiza watendji na wataalamu kusimamia miradi na fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita ili iweze kuisha kwa wakati
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Abdallah Hamis Ulega(MB) amezindua Miradi Miwili ya Maendeleo na kuweka Jiwe la Msingi mradi mmoja na kukagua Mradi Mmoja wa maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga yenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 3.Akizungumza Kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika tarehe 18/9/2024 katika viwanja vya Kituo cha Afya Ifingo Mheshimiwa Ulega amesema amefarijika kuona maendeleo Makubwa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo imepokea fedha kutoka Serikali Kuu, Halmashauri ya Mji Mafinga na kikubwa zaidi uchangiaji wa nguvu za wananchi katika utekelezaji wa Miradi hiyo.“ Nimeweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Rungemba jengo ambalo lilianza ujenzi kwa kuibuliwa na wananchi kwa nguvu zao wenye thamani ya shilingi Milioni 40 na Halmashauri ime jenga kwa mapato yake ya ndani shilingi Milioni 77. Hili na jambo la kujifunza.”Nitafikisha salamu hizi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa wananchi wa Mafinga wanafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wanatekeleza Miradi ya Maendeleo kwa juhudi zao na hivyo kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais na kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo la Mji Mafinga.Miradi iliyotembelewa na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo Mhe Abdallah Ulega (MB) ni;-Kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Zahanati ya Rungemba, Uzinduzi wa Shule Mpya ya Kata Mtaa wa Ndolezi Kata ya Boma ( SEQUIP), Kuzindua madarasa mawili katika Shule ya Msingi Kikombo na kutembelea ujenzi wa nyumba ya walimu(2 in 1) kupitia Mradi wa SEQUIPKatika Ziara hiyo Mbunge wa JimboLa Mafinga Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi amekabidhi vitanda 6 katika Zahanati ya Rungemba kwaajili ya jengo la mama na mtoto kuunga mkono juhudi za Serikali na wananchi walioibua mradi huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.