Halmashauri ya wilaya ya Kilolo imejipanga kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kuwahakikishia ajira ya kudumu.
Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo, Vallence Kihwaga alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari baada ya kutembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Kilolo.
Kihwaga alisema “Halmashauri ya wilaya ya Kilolo inaendelea kutekeleza mpango wa kuwavutia vijana ili wajiingize katika shughuli za kilimo na ufugaji. Vijana wengi wamekuwa wakizipa kisogo shughuli za kilimo na ufugaji, hivyo Halmashauri yangu inaendelea kuwavutia vijana wengi kujiingiza katika kilimo”. Aliongeza kuwa Halmashauri yake imetenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa katika maonesho ya Nanenane mwaka 2018 Halmashauri yake itapeleka wakulima wa kutosha kutoka kila Kata kujifunza ili wakawe chachu ya mabadiliko ya sekta ya kilimo na mifugo wilayani Kilolo. “Msimu huu, Halmashauri tumeamua kuleta waheshimiwa Madiwani wote wa Halmashauri ili wanaporudi wakawe injini ya kusukuma shughuli za kilimo na mifugo kwa wananchi wanaowasimamia” alisema Kihwaga.
Maonesho ya shughuli za wakalima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.