Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa ulifanyika Nchini tarehe 24 Novemba, 2019. Idadi ya Halmashauri ambazo zilifanya Uchaguzi huo katika Mkoa wa Iringa ni mbili (2) ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Aidha, Halmashauri tatu (3) za Mji Mafinga, Mufindi DC na Iringa DC hazikufanya Uchaguzi huo kwani wagombea wote wa nafasi zote katika Halmashauri husika walipita bila kupingwa.
Maeneo yaliyofanya Uchaguzi katika Halmashauri tajwa ni kama ifuatavyo;
Ulifanyika Uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati ya Mtaa watano (5) (Kundi la Wanawake 2 na Kundi Mchanganyiko 3) ambapo Wagombea wote watano waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
Wenyeviti wote sita waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Katika uchaguzi huo, jumla ya Viongozi/Wajumbe 88 walichaguliwa katika Halmashauri hizo mbili. Aidha, washindi wote 88 waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM). Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa.
Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa,
Humphrey Kisika.
MUHTASARI WA TAKWIMU ZA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA, 2019 MKOA WA IRINGA
Muhtasari wa hali halisi ya Wagombea wa Uchaguzi tajwa katika Mkoa wa Iringa ilikuwa kama ifuatavyo;
NB:Jedwali linaloonesha idadi ya Wagombea waliopita bila kupingwa kwa kila nafasi ya Uongozi katika Halmashauri zote tano (5) za Mkoa wa Iringa na waliochaguliwa tarehe 24 Novemba, 2019 ni kama ilivyoamabatishwa. Aidha, Wagombea wote waliopita bila kupingwa na waliochaguliwa wanatoka CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
Imetolewa na Ofisi ya Habari na Mawasiliano,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa,
Humphrey Kisika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.