Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ametoa rai kwa vijana nchini kufanya juhudi ya kujikinga na maambukuzi ya virusi vya UKIMWI kwa kuzingatia masomo na kujiepusha na tabia hatarishi zitakazosababisha kupata maambukizi na kushindwa kufikia malengo yao.
Mhe Dendego amesema hayo wakati akifunga Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania SHIMIVUTA katika viwanja vya samora mjini iringa ambapo amesema kuwa vijana ndio taifa la leo na vijana ndio nguvu kazi ya taifa hivyo pindi watakapopata maambukizi ya UKIMWI nguvu kazi ya taifa itapungua .
Aidha Dendego amewahimiza vijana kuendelea kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuendelea kuimarisha afya zao na kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Takribani washiriki 800 kutoka vyuo vya elimu nchini wameshiriki katika mashindano hayo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.