WANANCHI katika Mikoa ya Iringa, Tanga, Lindi na Geita wanatarajia kunufaika na Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishwaji wa Jamii na Ufunguaji wa fursa za kijamii na kiuchumi (RISE), ambapo zaidi ya shilingi bilioni 822 zitatumika kuboresha miundombinu ya barabara vijijini.
Mhe, halima Dendego Mkuu wa Mkoa Iringa amesema kuwa kusaini Kwa mikataba hii ni faraja kubwa Kwa wananchi wake kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu sana Kwa sababu ujenzi wa barabara hizo zitakuza uchumi wa wananchi wangu na pia mazao kufika Kwa wakati sokoni na viwandani, tofauti na sasa hususani kipindi cha mvua magari mengi yanakwama na kukaa muda mrefu na kusababisha wakulima kupata hasara kubwa.
Hata hivyo amewataka wananchi kushirikiana na wakandarasi hao na amewaonya wale wasio waaminifu hata chukua hatua Kali dhidi yao.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi na usimamizi baina ya TARURA na wakandarasi wa ujenzi na usimamizi wa mradi wa RISE iliyofanyika Mkoani Iringa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki (Mb), amesema, mradi huo wa RISE unaenda kuwakomboa wananchi hasa waishio vijijini kwa kuwafungulia fursa za kijamii na kiuchumi.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TARURA imekuwa ikifanya jitihada za dhati kuhakikisha kuwa inaboresha barabara za vijijini ili ziweze kupitika muda wote wa mwaka na ndiyo maana tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aingie madarakani Bajeti ya TARURA imeongezeka kwa takribani mara tatu kutoka bilioni 200 mwaka 2021 hadi bilioni 836 kwa mwaka 2023/2024.
Aidha, amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwajali watanzania wa hali ya chini na kueleza kuwa hawana cha kumlipa bali waendelee kumuunga mkono kwa hali na mali aendelee kuwatumikia.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, amesema kuwa lengo la mradi wa (RISE) ni kuboresha barabara za vijijini, kutoa fursa za ajira kwa wananchi katika maeneo ya vijijini yaliyochaguliwa na kujenga uwezo wa kitaasisi katika usimamizi endelevu wa barabara za vijijini kwa kutumia mbinu za ushirikishwaji wa jamii.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.