• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

MIKATABA 18 YA UJENZI WA BARABARA YASAINIWA IRINGA

Posted on: February 26th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Jumla ya mikataba 18 imesainiwa na wazabuni walioshinda zabuni yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 mkoani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa Wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa wa Iringa, Mhandisi Juma Wambura katika taarifa fupi ya TARURA iliyowasilikswa kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hafla fupi ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa barabara na vivuko baina ya TARURA na wakandarasi katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa jana.

Mhandisi Wambura alisema TARURA mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya halmashauri zote za mkoa. “Mhe. mkuu wa mkoa, TARURA Mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya halmashauri zote za mkoa jumla ya zabuni 26 zenye thamani ya shilingi bilioni 6.5 ambayo leo utaishuhudia mikataba 18 ikisainiwa na wazabuni walioshinda baada ya mchakato mzima wa manunuzi kukamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 3.56” alisema mhandisi Wambura. Alisema kuwa mikataba minane itasainiwa baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.

Mratibu wa TARURA mkoa aliwaasa wazabuni hao kutekeleza miradi hiyo kwa weledi na ufanisi mkubwa pasipo kuchelewesha kama utaratibu wa miaka ya nyuma ulivyokuwa. “Aidha, ninawakumbusha wazabuni kuacha mazoea ya kutekeleza kazi chini ya kiwango kwa visingizio mbalimbali. TARURA haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayezembea katika utekelezaji wa miradi hii” alisema mratibu wa TARURA. Aliwahakikishia wakandarasi kupata ushirikiano unaostahili katika kutekeleza majukumu yao.

Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya wakala za serikali sura 245 na kutangazwa katika Gazeti la serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017.

=30=

Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA GRUMA 2025

    July 05, 2025
  • KUELEKEA MBIO ZA THE GREAT RUAHA MARATHON

    July 01, 2025
  • MAAFISA ELIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA MICHEZO MASHULENI

    June 29, 2025
  • MASHINDANO YA UMITASHUMTA NA UMISSETA 2025 YACHAGIZA UCHUMI WA IRINGA.

    June 29, 2025
  • Tazama zote

Video

MAENDELEO KWA SASA BILA MAWASILIANO HAYAWEZEKANI- RC KHERI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.