Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (Mb), leo Julai 05, 2025 akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James wameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon (GRUMA 2025) zilizoanzia na kuishia kwenye eneo la Ibuguziwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, mkoani Iringa Akizungumza katika tukio hilo, Mhe Majaliwa ametoa wito kwa waratibu wa mbio hizo kuweka mikakati ya kuzifanya ziwe za kimataifa ili ziweze kukutanisha raia wa mataifa mbalimbali duniani. Lengo la Mbio hizo ni kuhamasisha uhifadhi wa mazingira wa Mto Ruaha Mkuu ambao ni uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuifanya jamii kuona umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali za asili. l
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.