• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • UTALII IRINGA
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

WANAFUNZI WANUFAIKA WA TASAF WATAKIWA KUWASHIRIKISHA WALIMU MASUALA YA TAALUMA

Posted on: December 5th, 2017


Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Wanafunzi wanufaika wa mpango wa kunusuku kaya masikini nchini (TASAF) kupitia ruzuku ya elimu wametakiwa kuwashirikisha walimu katika masuala yanayohusu taaluma na ustawi wao ili waweze kufaulu.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akiongea na wanafunzi wanufaika wa TASAF wa shule ya msingi Kitwiru iliyopo Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa hivi karibuni.

Ayubu alisema “watoto wangu mpo hapa kwa ajili ya kusoma na wote kufaulu, si ndiyo. Walimu wenu wapo hapa kwa ajili ya kuwafundisha na kuwasaidia kufaulu hivyo msiwaogope. Wafuateni kwa ushauri na maelekezo ili muweze kusoma vizuri na wote kufaulu, sawa”. Alisema kuwa serikali inatoa fedha kwa wanafunzi hao kiasi cha shilingi 2,000 kwa mwezi ili waweze kununua mahitaji ya muhimu ya shule. Serikali inataka kuona kila mtoto wa kitanzania anasoma vizuri ili aweze kujitegemea na kuchangia katika kukuza pato la Taifa.

Nae mratibu wa TASAF Mkoa wa Iringa, William kingazi aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwa wasikivu kwa walimu na wazazi. “Nyie wanafunzi lazima muwe na ndoto kwamba mtakapomaliza masomo mnataka kuwa watu wa aina gani. Ndoto hizo ziwasaidie kusoma kwa bidii ili muweze kuzifikia” alisema Kingazi. Aidha, aliwataka walimu kuwafuatilia wazazi wanufaika wa mpango wa TASAF ili waweze kuwanunulia watoto sare za shule kwa wale ambazo sare zao zimechanika ili wasijione tofauti na wengine.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa alifanya ziara maalum ya ufuatiliaji kwa wanafunzi wanufaika wa mpango wa TASAF kupitia elimu katika Manispaa ya Iringa kujifunza changamoto zinazowakabili. Katika ziara hiyo aliambatana na mratibu wa TASAF Mkoa, afisa mipango, mhasibu, mkaguzi wa ndani na afisa habari.

=30=



Matangazo

  • JOINING INSTRUCTION SHULE ZA SEKONDARI ZA SERIKALI MKOA WA IRINGA 2021 December 15, 2020
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA IRINGA 2021 December 18, 2020
  • Ratiba ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa Mwezi Machi March 08, 2019
  • Ratiba ya Mh. Mkuu wa Mkoa kwa Mwezi Aprili April 04, 2019
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkuu wa Mkoa Ally Hapi na Katibu Tawala Mkoa Bi, Happiness Seneda, pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama

    June 11, 2020
  • Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Aongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani Kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya Mufindi Tarehe 28 Mei, 2020

    May 28, 2020
  • Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi Aongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani Kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Mji wa Mafinga Tarehe 22 Mei, 2020.

    May 22, 2020
  • Mh. Hapi aongoza kikao kujadili Hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

    May 15, 2020
  • Tazama zote

Video

Wanasiasa uchwara wanapotosha jamii kuhusu corona
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Pawaga Road

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, Iringa

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2019, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.