Katika Kuhakikisha Iringa inaendelea kujitangaza kuwa ndio lango kuu la Utalii Kusini na shughuli nyinginezo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba amesema kuwa kwa sasa Mkoa unaanziasha Iringa Festival likiwa na lengo la kuacha kuutangaza utalii tu bali kuangazia fursa za uzalishaji mali zinazofanywa Mkoani Iringa kwa lengo la kupata maendeleo.Mhe. Serukamba ameyasema hayo leo Juni 11,2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisini kwake wakati akizungumza na Wafanyabishara na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo amesema kuwa lengo lingine la kuanzisha Iringa Festival ni kuhakikisha Tanzania nzima inafahamu fursa zinazopatikana Iringa na kupata Wateja na Wawekezaji .Naye Mkurugenzi na Mtaalam wa ukuzaji wa uchumi wa kampuni ya Kikashi Tanzania Limited ,Zachy Mbenna ameeleza kuwa Iringa iliangaliwa kwa kuona haja ya kutambua fursa za uwekezaji, biashara na utalii uliopo Iringa na kuelekea maendeleo ya dunia katika nyanja ya kisiasa na kijamii.Katika hatua nyingine Mbenna amesema moja ya sababu ya kuanzisha Iringa festival ni kutaka Iringa kuwa kitovu cha uwekezaji katika Tanzania nzima ambapo ili kufanikiwa kufanya Iringa festival itabidi iambatane na maonesho ya utalii wa Iringa ,ngoma za asili, maonesho ya bidhaa, vyakula vya asili ,burudani na zoezi la mbio ambalo litawapitisha wakimbiaji katika maeneo ya vivutio yatakayoshiriki na Wafanyabiashara, Wadau mbalimbali wa biashara ,Wadhamini ,Wasanini ,Wapikaji wa vyakula ambapo kutakuwa na gharama ya ushiriki maonesho hayo itatangazwa muda ukifika.Hata hivyo Katibu Mbenna amefafanua kuwa kutakuwa na mashindano ya kuchuma chai ambapo lengo ni kuonyesha ulimwengu kuwa Mkoani Iringa katika eneo la mufindi kuna ulimaji wa zao la chai ili kuweza kuleta ushiriki wa Makampuni makubwa na kufanyika uwekezaji.Kwa upande wao Wafanyabiashara mbalimbali wamelipongeza suala hilo huku kila mmoja akitoa maoni yao pamoja na kuongeza uaminifu katika kila huduma iitakayotolewa na Wafanyabiashara.Aidha Iringa Festivals itabeba taswira ya matukio yaliyokuwa yanafanyika katika hafla ya Utalii Karibu Kusini ambayo imezoeleka hufanyika kila mwisho mwa mwaka .Sasa Iringa Festivals inatarajiwa kufanyika mwezi wa nane ,2024 ambapo kauli mbiu yake inatarajiwa kuwa "TWIWONE Iringa yenye fursa lukuki " .#IringaLangolaUtaliiKusini
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.