• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

IRINGA IMEANDAA MPANGO WA KUBORESHA UTALII

Posted on: January 18th, 2018


Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Mkoa wa Iringa umeandaa mpango wa kuboresha maonesho ya utalii karibu kusini ili kuweza kuwavutia watalii wengi kutembelea vivutio vya utalii na kufurahia mandhari iliyopo katika vivutio hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi ya Mkoa wa Iringa kwa wajumbe kutoka chuo cha Taifa cha ulinzi waliotembelea Mkoa wa Iringa kwa ziara ya mafunzo.

Masenza alisema kuwa Mkoa wa Iringa ni kitovu cha utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini. Maonesho ya utalii karibu kusini yanatumika kukuza sekta ya utalii kwa mikoa ya nyanda za juu kusini. “Maonesho ya utalii karibu Kusini yanatumika kama mkakati maalum wa kufungua sekta ya utalii kwa ukanda wa Kusini ambao umejaa fursa na vivutio vya kipee katika utalii. Alitolea mfano maporomoko ya maji ya Kihansi ambapo wanapatikana vyura wa kipekee wanaozaa tofauti na vyura wengine wanaotaga mayai.

Mkoa wa Iringa ukiwa mratibu umeandaa mipango ya kuboresha maonesho haya kwa kutenga eneo la Kihesa Kilolo kama eneo maalum kwa ajili ya maonesho ya utalii karibu kusini. Eneo hili litatumiwa na wadau wa utalii na wadau wa maendeleo kujenga miundombinu kwa ajili ya kuonesha huduma na bidhaa za sekta ya utalii” alisema Masenza.

Mkoa wa Iringa ulifanya maonesho ya kuendeleza utalii ya karibu Kusini kwa miaka miwili mfululizo (mwaka 2016 na 2017) kwa kushirikisha mikoa ya nyanda za juu kusini ya Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Songwe, Rukwa na Katavi.

Akitoa neno la shukrani, kiongozi wa wajumbe kutoka chuo cha Taifa cha ulinzi Capt. Msafiri Hamisi alipongeza kwa mapokezi ya Mkoa na kazi zinazofanywa na Mkoa za kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo. Aidha, aliahidi wanafunzi wa chuo cha Taifa cha ulinzi kuwa balozi wazuri kwa mkoa wa Iringa.

=30=



Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.