• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

JAMII KUJENGA UTAMADUNI WA UADILIFU IRINGA

Posted on: July 19th, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, IRINGA

Jamii imetakiwa kujenga utamaduni wa uadilifu katika kuitikia sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kanuni za serikali za mitaa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akifungua semina kwa waheshimiwa madiwani na wakuu wa idara na vitengo wanawake katika Mkoa wa Iringa kuhusu maadili ya viongozi wa umma katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.

Masenza alisema kuwa uadilifu sharti ujengwe ndani ya jamii ili kuwa utamaduni wa nchi. “Sheria ya maadili ya viongozi wa umma, kanuni za serikali za mitaa  pamoja na vyombo vya kusimamia utawala bora pekee haviwezi kufanikisha suala la kukuza na kusimamia maadili. Jukumu la kukuza na kusimamia maadili ya viongozi wa umma linahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya viongozi, wananchi na wadau mbalimbali” alisema Masenza.

Viongozi wanawake wana dhamana na ushawishi mkubwa katika jamii, hivyo wanapashwa kuongoza katika juhudi za kukuza maadili kwa vitendo. “Hatuna budi kuwahamasisha wananchi kuchukia vitendo vya ukiukwaji maadili na kuwakataa viongozi wasio waadilifu.  Ni matumaini yangu kuwa elimu mtakayoipata katika semina hii mtaitoa pia kwa wanawake wengine katika Halmashauri zenu,  wananchi katika Kata zenu na, Mitaa ambako mnatekeleza majukumu yenu ya kila siku” alisema Masenza.

Moja ya misingi ya demokrasia ni kuwa na Serikali inayowajibika kwa wananchi na yenye viongozi wanaowatumikia wananchi kwa uadilifu, alisema. Wananchi wanategemea viongozi watatumia nafasi zao za uongozi kuwaletea maendeleo na sio vinginevyo, aliongeza. “Sote tunafahamu kwamba uongozi ni dhamana. Kiongozi yeyote, awe ni wa kuchaguliwa ama wa kuteuliwa, amekabidhiwa madaraka na wananchi” alisema. Viongozi wa kisiasa na watumishi wa umma wanatakiwa kutumia nyadhifa zao kwa manufaa ya wananchi.

=30=


Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.