Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mpaka kufikia Disemba 30, 2027 iwe imekamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa machinjio ya kisasa ya Ngelewala iliyopo katika Halmashauri hiyo ambayo Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 2 ili kusaidia kutoa huduma kwa wananchi na kuchagiza ukuaji wa uchumi.
Akisoma maazimio kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Machi,17,2025,Mhe. Omary Kiguo, ambaye ni Mbunge wa Kilindi Tanga amesema kuwa mradi huo ukamilike katika kipindi pendekezwa na kuondoshwa kwa dosari zote za kiukaguzi walizozikuta katika mradi.
Machinjio hiyo ilianza kujengwa toka mwaka 2008 na ina uwezo wa kuchinja ng’ombe 100 na mbuzi 200 kwa siku.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.