Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa iringa, amezindua kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia huku akihimiza wananchi kijitokeza katika kampeni hiyo itakayosaidia kutatua changamoto zao
Ameyasema hayo Novemba 10,2024 kwenye viwanja vya Mwembetogwa vilivyopo Mjini Iringa.
Mhe. Ngwada ameanza kwa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluh Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha Kampeni hiyo inayoenda kuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwani wananchi wengi watajitokeza katika maeneo mbalimbali na kutatuliwa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.