• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

KILIMO KINACHANGIA ASILIMIA 85 YA PATO LA MKOA IRINGA.

Posted on: January 2nd, 2018


Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

Sekta ya kilimo inachangia katika usalama wa chakula na utoaji ajira na uchumi wa Mkoa wa Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi ya Mkoa wa Iringa kwa wajumbe kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa waliofanya ziara ya mafunzo ya siku tano mkoani Iringa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa jana.

Masenza alisema “sekta ya kilimo katika Mkoa ni muhimili mkuu wa uchumi na inachangia katika usalama wa chakula na utoaji wa ajira. Sekta hii inachangia takribani asilimia 85 ya pato la Mkoa kwa mujibu wa wasifu wa kiuchumi na Kijamii, mwaka 2013”. Alisema kuwa lengo la Mkoa ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na chakula cha kutosha, wanaongeza kipato na uhakika wa upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda.

Akiongelea sekta ya mifugo na uvuvi, mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa una mashamba makubwa ya mifugo 20 yanayomilikiwa na serikali na watu binafsi. Alisema kuwa mashamba hayo huzalisha maziwa, mitamba na madume bora.

”Mkoa wa Iringa hadi kufikia Juni, 2017 ulikuwa na jumla ya ng’ombe 330,372, mbuzi 160,227, kondoo 62,475, nguruwe 109,131 na kuku wapatao 1,341,718 na eneo linalotumika kwa malisho ni jumla ya hekta 209,003” alisema mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wa uvuvi, alisema kuwa Mkoa una mabwawa madogo 1,893 yaliyochimbwa yanayotumiwa kwa shughuli za uvuvi. Alisema kuwa Mkoa una wavuvi 5,807 ambao hufanya shughuli za uvuvi kama mtu mmoja mmoja na katika vikundi. Mavuno ya samaki yamekuwa yakiongezeka kutoka Tani 913.50 mwaka 2011/2012 hadi kufikia Tani 1,186.99 mwaka 2014/15.

Kwa matokeo ya Sensa ya mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na watu 941,238 kati ya hao wanaume walikuwa 452,052 na wanawake 489,186 na wastani wa ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka ni asilimia 1.1. Makadirio ya idadi ya watu kwa mwaka 2017 ni watu 1,000,040; wanaume wakiwa 480,293 na wanawake 519,747.

=30=



Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.