Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Joachim Nyingo Ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo amefunga mafunzo yaliyotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoani Iringa huku akiwataka watendaji kwenda kuwa chachu ya maendeleo kwenye jamii baada ya kupata mafunzo hayo.
Ameyasema hayo l Agosti 12,2024 kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambapo Mhe. Nyingo amesema kutokana na mafunzo waliyoyapata wakawe chachu ya maendeleo kwa kuhakikisha wanasimamia suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ujenzi wa vituo vya afya pamoja na madarasa.
Aidha Mhe. Nyingo amewasisitiza watendaji katika maeneo yao kuhakikisha wanaimarisha suala la ulinzi na usalama kwa wananchi na mali zao.
Mafunzo haya yameanza tarehe 11,2024 na kufungwa tarehe 12/08/2024 ambapo Maafisa Tarafa na Watendaji kata wote Mkoani Iringa wameudhuria katika mafunzo hayo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.