Mhe Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego amefanya ziara katika shamba la Shirika la Farm for The Future lililopo katika eneo la Masukanzi Ilula na kujionea shughuli mbalimbali za kilimo na ufugaji. Akiwa katika shamba hilo Mhe Mkuu wa Mkoa Halima Dendego ambaye aliambatana na Meneja Mradi wa Farm for The Future Bw. Osmund Ueland amepanda mche wa zao la karanga mti maarufu kama Macademia. Mhe. Dendego pia amejionea na kupata maelezo jinsi ya uendeshaji wa kilimo cha zao la karanga mti na jinsi kinavyoweza kumkwamua mkulima kutoka katika lindi la umasikini wa kipato. Akiwa shambani hapo pia Mhe. Dendego ameona na kupata maelezo ya ufugaji wa samaki na mbuzi wa biashara.
Imetolewa na Afisa habari na uhusiano, itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.