Mhe. Suleimani Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ameongoza maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo kitaifa yamefanyika mkoani iringa.
Awali Akitoa taarifa ya Mkoa Mhe. Halima O. Dendego Mkuu wa mkoa wa iringa amemwambia mhe. Jafo kuwa mkoa wa iringa upo salama na pia kupitia Muungano Mkoa umekuwa na Maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali
Aidha katika maadhimisho haya Mkuu wa Mkoa Kwa kushirikiana na viongozi wengine wameshiriki katika zoezi la kupanda miti katika shule ambapo miti elfu 89 imepandwa Kwa lengo la kutunza mazingira yetu.
Akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali Mhe. Jafo amempongeza Mhe. Mkuu wa mkoa iringa Kwa kuadhimisha sherehe hizo Kwa aina yake ya kuandaa ( bonanza) Kwa kufanya hivi ni Moja ya njia ya kudumisha umoja na mshikamani kwani michezo inaleta watu pamoja lakini pia Kwa kufanya hivi pia tunaunga juhudi za mhe. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele kusahimiza michezo. Kwa upande mwingine Mhe. Jafo ameendelea kuwahimiza wananchi kuendelea kuwa na umoja na Mshikamano.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.