Mheshimiwa Hapi ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kupata hati safi tangu ilipoanzishwa, kwani ni maelekezo ya Serikali kuwa katika Halmashauri zote lazima zijibu hoja za Mkaguzi wa Serikali.
Mheshimiwa Hapi ameendelea kusema kuwa, Mji wa Mafinga nimekuja mara nyingi, hivyo naujua vizuri na Madiwani hawa nimefanya nao kazi kwa ushirikiano mkubwa sana. Kwa kweli mnafanya vizuri kila jambo, kama elimu, mapato, miradi mbalimbali kama vituo vya afya na kupelekea kupata hati safi.
Hapi amesema katika ziara yangu ya #IringaMpya nimeona kero ni chache sana, ni kero 27 tu ndizo zilizokuwepo, hii inaonesha kuwa mnafanya kazi vizuri. Mshikamano na kujituma ndiyo mafanikio yenu. Katika hoja 33 zimebaki hoja 5 tu, naomba wataalamu wazishughulikie ili hoja hizi zifutwe.
Mheshimiwa Hapi amewakumbusha kuwa, Vifaa vilivyoletwa vya kiasi cha Tsh. 15 milioni kwa ajili ya Kituo cha Afya Ihongole, vianze kufanya kazi ili wananchi waweze kupata huduma bora. Jambo la madeni ya watmishi na wakandarasi siyo mbaya sana, ninaomba yalipwe hasa kwa watumishi ili wapate morali ya kufanya kazi. Pia sekta ya elimu imekuwa na changamoto kutokana na idadi ya uandikishaji, hivyo agenda yenu kuu katika vikao iwe ni elimu, kuongeza madarasa, kuweka benki ya matofali ili kusiwepo na upungufu. Katika Mkoa wetu kimapato tuko vizuri sana kwa Halmashauri zote.
Serikali ya Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ili kutekeleza majukumu. Halmashauri hii imejigawa ili kurahisha utoaji wa huduma kwa wananchi. Tuendelee kushirikiana kutatua shida za wananchi ili kusiwepo na vita kati ya Mafinga Mji na Halmashauri ya Wilaya Mufindi.
Nawaomba Madiwani kuhamasisha wananchi kuchangia katika mfuko wa CHF iliyoboreshwa kwani ni mkombozi kwa wananchi, hivyo watu wajiunge kwa wingi katika mfuko huu.
Nawaomba mambo makubwa mawili:-
Mwisho Mheshimiwa Hapi amewatakia kila la heri katika uchaguzi mkuu ujao.
Pia Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Happiness Seneda naye alikuwa na haya ya kusema, kwanza kwa kuwapongeza Mafinga Mji kwa kuhamia katika jengo lao jipya, pili aliwapongeza kwa kupata kupata hati safi, tatu amewapongeza kwa ukusanyaji mzuri wa mapato na kuw Halmashauri kushika nafasi ya 19 kati ya Halmashauri 185 nchini. Nne amewapongeza kwa kujibu vizuri hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, tano amewapongeza kwa kutokuwa na madeni kwa Madiwani.
Pamoja na pongezi hizi, Mheshimiwa Katibu Tawala amewaomba kuendelea kushughulikia hoja za kamati, na kutosubiri hadi waitwe na kamati ya LAAC. Amesema kwa kutumia Timu ya Menejimenti ya Halmashauri (Council Management Team – CMT) kuhakikisha hoja zote zinajibiwa kikamilifu. Pia amesisitiza kushughulikia hoja za Mkaguzi wa Ndani, kwni kufanya hivi inapunguza hoja za LAAC.
Mwisho ameomba tuendelee kupambana na janga la corona, huku tukichukua tahadhari na kuondoa hofu. Pia kuhakikisha tunafanya kazi ili uchumi wetu usishuke, hasa katika fursa za kilimo, na kuwatakia heri katika uchaguzi ujao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.