Mheshimiwa Hapi pamoja na salamu mbalimbali alianza kwa Mwenyezimungu kwa rehema alizotujali, na kuwepo katika Baraza la Mwisho la Madiwani kwa kujadili hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
Mheshimiwa Hapi amesema, Serikali imetoa maelekezo ya matumizi ya fedha za ziweze kukaguliwa, pia ilitoa kwa Kamati ya Bunge kukagua mahesabu na miradi mbalimbali. Mheshimiwa Hapi amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kusimamia vema kwa kadiri ya taratibu zinavyotakiwa, pia Baraza la Madiwani, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na watendaji wote wa Halmashauri kwa kupata hati safi. Ushirikiano wao ndiyo umewafikisha hapa tulipo na kuwaasa kutojibweteka kwa vile wamepata hati safi.
Katika hoja 36 na 11 za miaka ya nyuma na kuleta jumla ya hoja 47, na hoja
28 zimefutwa na kubakia hoja 19, pia maagizo ya LAAC kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo kabla ya mwaka wa fedha kwisha.
Kw upande wa madeni; Halmashauri ina utaratibu wa kukusanya mapato kwa mashine na kupeleka benki, kiasi cha Tsh. 232 milioni hazijaenda benki kama taratibu zinavyosema. Wale ambao walikusanya pesa hawajapeleka benki ili ziwe kwenye mfumo wafanye haraka iwezekanavyo kupeleka benki. Kuna watu waliofanya ubadhilifu wachukuliwe hatua haraka sana bila kuwaonea haya. Maana kuna utaratibu kuwa, mtu akifanya ubadhilifu mnamuambia urudishe au mnakata kwenye mshahara wake hadi deni litakapokwisha, hii tabia sitaki kuisikia tena, wachukuliwe hatua kali za kisheria. Halmashauri ina madeni ya watumishi na wakandarasi, kiasi cha Tsh. 395.1 milioni. Lipeni madeni haya hasa watumishi ili wapate moyo wa kufanya kazi kwa bidii.
Tulipokea vifaa kutoka MSD kwa ajili ya hospitali ya Malangali, baadhi ya vifaa havijaanza kutumika, nahitaji vianze kutumika kwa kuwapa wananchi huduma bora. Pia usimamizi wa mali za Halmashauri, kuna magari hayatumiki au ni chakavu, kama yanatengenezeka basi yatengenezwe na kam haiwezekani yaondolewe kwenye mfumo na yasisomeke.
Nawapongeza kwa kutoa 10% kwa ajili ya mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu, nawapngeza sana kwa kujali vikundi. Endeleeni kusimamia matumizi ya fedha hasa kwenye akaunti ya Amana.
Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana kuleta miradi mikubwa kama maji, hospitali, barabara, elimu n.k. Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu wan chi, hakikisheni miradi yote inakamilika ili kusiwepo na maswali kwa wananchi hasa upande wa elimu kwani uandikishaji ni mkubwa sana.
Pia nawapongeza kwa kukusanya mapato kwa kufikia 88% hadi kufikia leo. Sote tunajua bila mapato hana huduma. Mkurugenzi na timu yako endeleeni kusimamia, kabla ya kufika mwisho wa mwaka iwe imefika 100%. Mkurugenzi kaza uzi katika suala hili, asitokee mtu anakwepa kulipa ushuru, kodi ni lazima vilipwe. Nasisitiza kufuata taratibu za fedha na manunuzi, hii itasaidia kudhibiti hoja. Pia nawapongeza kwa kulipa madeni ya madiwani.
Maagizo:
Mwisho Mwenyekiti wa Halmashauri alitoa maombi kwa Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.