Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Queen Cuthbert Sendiga ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa Mkoa wa Iringa kusimamia utekelezaji wa sheria inayowataka wamiliki wote wa majengo yanayotumiwa na watu wengi kuweka mabango na kutenga maeneo ya kuvutia bidhaa za tumbaku.
Mhe:Queen Sendiga ameyasema hayo aliposhiriki kikao kazi kilichoandaliwa na mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) kilicholenga kupeana uelewa wa shughuli za udhibiti wa bidhaa za tumbaku kwa viongozi wa ngazi ya Mkoa na Manispaa ya Iringa.
Aidha amewataka wawakilishi wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa wakawe mstari wa mbele katika kutekeleza maagizo hayo muhimu na kufikisha taarifa hizi kwa wafanyabiashara wote mkoani Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.