Katika ufunguzi huo Mhe.Halima Dendego amewataka viongozi wote kushirikiana vyema katika kutatua Changamoto Mbalimbali zinazowakabiki wananchi na Wakurugenzi kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuendelea kubainisha vyanzo vipya vya mapato.
Piah Mhe.Halima Dendego amewataka wafanyabiashara wadogo waliovamia eneo la ndani ya makaburi ya Mlandege ili kujenga vibanda vya biashara kuondoka mara Moja kwani ni kinyume na maadili na kuiagiza Manispaa ya Iringa kujenga kuanza mara Moja ujenzi wa ukuta utakaozunguka eneo hilo
"lile ni eneo Takatifu wenzetu wamepumzika na sisi tutaendelea kupumzika pale Leo watu wanapiga makofi kuona vijana wale wamejenga kwenye makaburi ,sio sawa ni kinyume na Mila na desturi ,hatutokubali jambo la kipuuzi kama lile,siasa hizi zisitufanye tukapoteza utu wetu mbele ya mungu adhabu yake ni kali"
Ikumbukwe March 10, 2023 ilikuwa siku ya mwisho ya Wamachinga kupanga vitu vyao kwenye maeneo yasiyo rasmi katikati ya Mji na vibanda vyao viliondolewa na kuambiwa wahamie soko la Mlandege na Eneo la lavela Sehemu zilizoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Imetolewa na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.