*MKUU WA MKOA WA IRINGA MHE. SENDIGA AWASHUKIA MADEREVA NA MAKONDAKTA WA DALADALA KUWEKA VIFAA VYA KUHIFADHIA TAKA NDANI YA GARI*
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Qeen Sendiga amezindua kampeni ya Iringa safi iliyofanyika leo tarehe 26/6/2021 mara baada ya matembezi ya hiyari ya kuokota taka taka kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika masuala ya usafi na utuzaji wa Mazingira
Mh.Sendiga amewataka wananchi kutimiza wajibu wao wa kufanya usafi bila kusubiri kuhamasishwa na viongozi kwani usafi ni jukumu la kila mmoja
Aidha ametoa wito kwa madereva wa daladala na makondakta kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka katika gari zao ili kuepusha mlundikano wa taka katika eneo la stendi kuu ya zamani unasababishwa na baadhi yao kutupa taka eneo hilo jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi
Mh.Eliud Mvela ni Diwani wa Kata ya Mkimbizi akimuwakilisha Mstahiki Meya amesema kwa muda mrefu Manispaa ya Iringa inafanya vizuri katika mashindano ya usafi wa Mazingira ambayo hujumuisha Majiji,Miji, na Halmashauri zote nchini na imekuwa ikishika nafasi za juu za ushindi na kwa mwaka huu kutokana na mikakati iliyowekwa na Madiwani kwa kushirikiana na Menejimenti kwenye vikao vya ndani amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa Manispaa itashika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo
Abdon Mapunda ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na mkuu wa kitengo cha Mazingira amesema anapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ikiwemo kukamatwa kwa yeyote atakayeonekana kutupa taka hovyo na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja
Paulo Myovela ni mwenyekiti wa Envibright anasema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo ni upungufu wa vifaa na kuwaomba wadau kujitokeza kusaidia vifaa vitakavyorahisisha utendaji kazi ili kufikia malengo
Kampeni hiyo ya Iringa safi imezinduliwa leo na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwepo Waheshimiwa Madiwani,wakuu wa idara na vitengo na wadau Nipe fagio pamoja na Envibright.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.