Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh,Queen Sendiga leo tarehe 08.01.2022 amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya mkoa katika maeneo ya izazi na Pawaga ikiwa ni muendelezo wa ziara zilizopita katika kufanikisha kumalizika kwa miradi yote inayoendelea mkoani Iringa
Ziara ilianzia katika shule ya secondary Isimani ambapo mkuu wa mkoa alikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa mawili ya kisasa unaoendelea shuleni hapo na ziara ilifuatiwa na ukaguzi wa mradi wa maji wa izazi na baadae katika mradi wa maji wa pawaga ambapo Mh Queen Sendiga alikagua na kuelezwa juu ya maendeleo ya miradi ya maji ambayo ni shida kubwa katika maeneo hayo.
Ziara ilimalizika kwa mkutano wa hadhara ambao ulifanyika kata ya Itunundu Pawaga na ulikutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa wilaya , viongozi wa chama cha mapinduzi pamoja na madiwani ambao walijumuika na wananchi pamoja na Mkuu wa mkoa kwenye mkutano huo.aa
Mh mkuu wa mkoa amesifu viongozi wote wa chama na wa serikali kwa maendeleo ya miradi inayo tekelezwa katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madara 94 katika halamashauri hiyo amabayo itaenda kurahisisha utoaji wa elimu pamoja na kupeleka watoto shule kwa awamu moja tofauti na kipindi cha nyuma wakati kuna uhaba wa madarasa pamoja na miradi ya maji amabyo itaenda kupunguza shida ya maji katika kata hiyo.
Mkuu wa mkoa pia amemtaka Mkurugenzi kuhakikisha miradi hiyo inamalizika mapema na shida ya maji inatoweka katika kata hiyo na amesisitiza kuhakikisha wananchi wanatunza miundombinu hiyo ili shida ya maji isijitokeze maeneo hayo pamoja na uchangiaji wa maji hayo
“serikali inatumia gharama kubwa kuleta maji maeneo hayo tutunze miundombinu tuache ubinafsi ni dhambi , kuiharibu miundombinu makusudi ili ulishe mifugo ikiwa kijiji kingine wanakosa maji hiyo ni roho mabaya” amesema Mh. Queen Sendiga
Mh. Mkuu wa mkoa alizungumza na wananchi wa itunundu Pawaga swala la kupeleka watoto shule kwani madarasa ya yako tayari na kuandikisha ni bure hii ni baada ya takwimu kuonyesha kua uandikisha wa wanafinzi wa darasa la kwanza na awali kua mdogo kulingana na watoto wanao patikana katika maeneo hayo.
Mh. Queen Sendiga alihitimisha mkutano kwakuipongeza RUWASA kwa juhudi zao kuhakikisha maji yanafika kila sehem mkoani Iringa na kuisikiliza kero za wananchi wa pawaga ambapo kero kubwa ilikua ni maji kutoka kwa awamu pamoja marekebisho katika hospitali ya kata na akamtaka mkurugenzi pamoja na wataalamu wa maji kuhakikisha kero hizo zinatatuliwa kwa haraka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.