Jumla ya miradi 26 yenye thamani ya kiasi cha Bilioni 7,650,102,263 inatazamiwa kukaguliwa na mbio za mwenge mwaka 2019.Akipokea ujumbe huo wa mwenge Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Salum Hapi kutoka mkoa waMbeya amesema kwamba mwenge huo pia utatembelea shughuli 15 za maendeleo.
“Kati ya fedha hizo Bilioni 7.6,milioni 197,130,101 ni michango ya wananchi,shilingi milioni 304,671,600 ni michango ya Halmashauri ,huku shilingi Bilioni 6.3 ni michango kutoka serikali kuu na shilingi Bilioni 1,011,938,810 ni michango ya wadau wa maendeleo”alisema RC Hapi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Hapi amesema mwenge huo utakagua miradi mitatu iliyozinduliwa na mbio za mwenge za mwaka uliyopita ambapo viongozi watapokea taarifa za utoaji wa huduma katika maeneo husika.
Mhe.Hapi amesema serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya mwenge ya mwaka huu isemayo”Maji ni Haki ya kila mtu,tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”kwa kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa pamoja na upandaji wa miti na kuongeza kiwango cha wananchi wanaopata huduma ya maji vijijini na mijini.
“Kwa kuzingatia dhamira ya serikali wa awamu ya tano ya kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wote…hadi kufikia juni ya mwaka 2019 ulikuwa na jumla ya watu 748,114 sawa na asilimia 71.2% ya wakazi wote wa mkoa wa Iringa wanaopata huduma ya maji safi na salama”kwa upande wa mijini jumla ya watu 313,081 sawa na 82.6% ni watu 535,033 sawa na 70% wanapata huduma ya maji safi na salama”
Mwenge huo utakimbizwa katika Halmashauri tano na kukabidhiwa kwa mkoa wa Njombe baadae septemba 14.
Mkoa wa Iringa umekuwa mkoa wa 27 kutembelewa na mwenge kwa mwaka huu tangu ulipozindua mbio zake mapema mwezi april mwaka huu na WaziriMkuu Kassim Majaliwa Mkoani Songwe.
Imeandikwa na,
Afisa Habari wa Mkoa-Iringa
Humphrey Kisika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.