• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Iringa Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahala
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma ya Maji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Huduma za Kisheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Iringa
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Mufindi
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
    • Kilolo
      • Historia
      • Viongozi
      • Halmashauri zilizopo kwenye Wilaya
  • Halmashauri
    • Iringa MC
    • Mafinga Mji
    • Iringa DC
    • Kilolo DC
    • Mufindi DC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Viwanda na Biashara
    • Vivutio vya Kitalii
      • Fahari Yetu
      • CHOGELASAFARICAMP
      • Kitovu cha Utalii Nyanda za Juu Kusini
      • RUAHA HILLTOP
      • Hifadhi ya Taifa Ruaha
      • Udzungwa Mountains National Park
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Habari
    • Fomu
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • News Later
    • Matukio

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO 40 YA TSHS 24,427,360,696.40

Posted on: May 22nd, 2018

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Mwenge wa uhuru utatembelea miradi ya maendeleo 40 yenye thamani ya shilingi 24,427,360,696.40 mkoani Iringa na kutoa ujumbe maalum wa mwaka 2018.

Akitoa taarifa ya ujuo wa Mwenge wa uhuru kwa wananchi kupitia vyombo vya habari vya mkoa wa Iringa, mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa Mwenge wa uhuru utatembelea, kagua, kuzindua, kufungua na kuweka mawe ya msingi,  jumla ya miradi 40 ya maendeleo. Aliongeza kuwa miradi hiyo ina thamani ya shilingi 24,427,360,696.40. “Miradi hiyo inatoka sekta za elimu (10), afya (7), maji (4) maliasili (1), kilimo (5), viwanda viwili (2) uvuvi (1) na mapambano dhidi ya rushwa (4). Gharama za miradi hiyo zimetokana na michango ya wananchi shilingi 1,251,610,850.00, Serikali kuu shilingi 8,638,969,449.40, Halmashauri shilingi 253,564,461.00 na wadau wa maendeleo shilingi 14,283,215,936.00” alisema Masenza.    

Akiongelea ujumbe wa Mwenge wa uhuru mwaka 2018, mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mwenge wa uhuru utatoa ujumbe maalumu na ujumbe wa kudumu katika maeneo yote ambako utakimbizwa. Ujumbe maalumu wa Mwenge wa uhuru wa mwaka 2018 ni: ‘Elimu ni Ufunguo wa Maisha; Wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu’. Ujumbe huu unalenga kutilia mkazo umuhimu wa uwekezaji katika elimu unaofanywa na serikali pamoja na Wananchi ikiwa ni mkakati madhubuti katika kupiga vita umaskini na kujenga taifa lenye maendeleo ya viwanda alisema mkuu wa Mkoa.

Pamoja na kutoa ujumbe mahususi, Mwenge wa uhuru utaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya UKIMWI chini ya kauli mbiu isemayo ‘mwananchi jitambue; pima afya yako sasa’. Ujumbe mwingine aliutaja kuwa ni mapambano dhidi ya Malaria chini ya kauli mbiu isemayo ‘Shiriki kutokomeza Malaria kwa manufaa ya Jamii’.

Ujumbe mwingine ni mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya chini ya kauli mbiu isemayo ‘Tuwasikilize na kuwashauri watoto ili wasitumie dawa za kulevya’ na Mapambano ya kutokomeza Rushwa chini ya kauli mbiu isemayo:-‘Kataa Rushwa- Jenga Tanzania’.

Mwenge wa Uhuru utakimbizwa mkoani Iringa kwa siku tano na kukabidhiwa mkoani Njombe tarehe 28/5/2018.

=30=


Matangazo

  • No records found
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UKAGUZI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MUFINDI

    May 08, 2025
  • RC SERUKAMBA AHIMIZA UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI NA WATUMISHI

    May 07, 2025
  • MTIHANI MWEMA KIDATO CHA SITA

    May 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAKAMILISHA ZIARA MKOA WA IRINGA NA KUKABIDHIWA MKOA WA NJOMBE

    May 03, 2025
  • Tazama zote

Video

RC SERUKAMBA: WANANCHI PAWAGA FANYENI KAZI KWA BIDII.
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Iringa
  • PReM
  • Investment profile
  • Ajira za waalimu
  • Press release

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji Kidunia

world map hits counter

Jumla ya Watembeleaji

COUNTER-free

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga

    Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania

    Simu: +255 262 702 715

    Mobile:

    Barua pepe: ras@iringa.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.