Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, IRINGA
Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Iringa ametakiwa kuwasilisha orodha ya watu wote waliopora mali za ushirika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Agizo hilo lilitolewa na mwenyekiti wa Tume ya maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kamani jana alipokuwa akiongea na viongozi wa vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na vyama vya ushirika vya kilimo na masoko (AMKOS) katika ukumbi wa chuo cha ushirika Moshi tawi la Iringa.
Dkt Kamani alisema “Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Iringa, nataka orodha ya wote waliopora mali za ushirika. Serikali haiwezi kufumbia macho uporaji huo, lazima warudishe mali za ushirika na sheria kuchukua mkondo wake”. Aidha, alimtaka kuhakikisha watu waliofanya ubadhilifu wa mali za Soko Kuu SACCOS watafutwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mwenyekiti wa Tume ya maendeleo ya ushirika alisema kuwa muda wa dili umekwisha. “Serikali ya awamu ya tano, kupitia Ilani ya uchaguzi ya CCM imedhamiria kuhakikisha ushirika unasonga mbele. Hivyo, haitamvumilia mtu yeyoye mwenye nia ya kuwakisha juhudi za wanaushirika kujikomboa kupitia SACCOS” alisema Dkt Kamani.
Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ushirika wa akiba na mikopo (..) yatafanyika mkoani Iringa na kilele chake tarehe 18 Septemba, 2018 katika uwanja wa Kichangani mjini Iringa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.