Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mkono wa heri kwa watoto katika vituo vya kulea watoto wenye mahitaji maalum na wanaoishi katika Mazingira magumu Mkoani Iringa kwa kugawa Sadaka ya vyakula ikiwemo mbuzi, mchele, mafuta ya kupikia, unga, sabuni za kuogea na kufulia pamoja na vinywaji. Akizungumza wakati wa kugawa Sadaka hiyo katika kituo cha kulelea watoto cha Sisi ni Kesho children homes Nyororo, kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Nyumba yetu orphanage center Isimani na Amani Center katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Doris Kalasa amesema kuwa jamii inapaswa kuiga mfano huo mzuri kwa kuwajali watu wenye uhitaji kwa kuwa wananafasi ya kuishi kama binadamu wengine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2025, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.