Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewataka Wananchi kuendelea kuunga mkono Kazi anazozifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kwa kujenga na kuboresha miundombinu.Ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha NATUREZA kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ambapo amesema kuwa katika kipindi hiki wawekezaji wameendela kuwa wengi kwasababu ya uwepo mzuri ya miundombinu ya Barabara, umeme na maji vitu ambavyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amevifanya kwa kasi kubwa sana na kupelekea wawekezaji kufurahi kuwekeza nchini hapa.Pia Mhe.Serukamba ameendelea kuwahimiza viongozi wa Halmashauri kuhakikisha wanasimama vizuri na kwa uangalizi mkubwa viwanda vyote vilivyopo katika Halmashauri hiyo kwa kuatatua changamoto wananzokumbana nazo na kuhakikisha wawekezaji hao wanafuata sheria zote na kulipa kodi.Aidha Mhe. Serukamba ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuja kuwekeza mkoani Iringa na kuwahakikishia mazingira ya uwekezaji yapo na ni mazuri na Serikali ya Mkoa ipo tayari kuwapokea na kuwawekea mazingira mazuri.Nae Mbunge wa Viti maalumu Mhe. Ritha Kabati amemshukuru Muwekezaji huyo kwa kuja kuwekeza Wilayani hapo na kusema kuwa uwepo wa kiwanda hicho umekuwa chachu ya mafanikio na maendeleo ya wananchi, Mkoa na Taifa kwa ujumla huku akisema kwa sasa Wilaya ya Kilolo inakuwa ni Wilaya ya viwanda.Wananchi zaidi ya 200 wamepata ajira kupitia kiwanda hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.