Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego amemkabidhi Ofisi Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ambapo amemkabidhi nyaraka mbali mbali za muhimu kama kukamilisha mchakato wa sakata la wamachinga, na bajaji na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Mhe.Dendego amesema kuwa asilimia 90 ya Miradi ya maendeleo ipo katika hatua nzuri na wana Iringa ni wachapa kazi. Mhe.Serukamba anahamia Iringa akitokea Mkoa wa Singida akibadilishana na Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego anayeenda Mkoani Singida
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.