Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa akiwataka Wakuu wa Wilaya na wenyeviti wa vijiji kuwafuatilia kwa ukaribu maafisa ugani waliopo kwenye maeneo yao maana awaendi kuwasaidia wakulima na kutoa ushauri wa kitaalamu wao wana kaa tu ofisini hii aikubaliki hata kidogo maana inapelekea kupata mavuno machache ya mazao. Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Dendego amewataka Maafisa Ugani kuacha tabia ya kukaa ofisini na Badala yake kwenda kutoa Elimu kwa Wakulima kwa Lengo la Kukuza Sekta hiyo ya Kilimo "Sasa hivi ukienda Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati utawakuta watendaji wote kwenye maeneo yao ya kazi, ukienda shuleni utawakuta walimu, lakini hawa maafisa ugani hawaendi shambani kwa Mkulima na kutoa elimu ya Kilimo wakati serikali imewapatia vitendea kazi Kama pikipiki na vifaa vya kupima udongo. sikubaliani na hili" Mhe. Dendego Mkuu wa Mkoa Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.