Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amehimiza Wazazi na Walezi Nchini kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu na kuwahimiza watoto hao juu ya Umuhimu wa Elimu kwani Elimu ndio Nguzo ya maendeleo ya jamii na UchumiAmeyasema hayo leo Septemba 20,2024 wakati akihutubia kwenye mahafali ya wanafunzi wa Shule ya Real Hope iliyopo katika Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi.Mhe Serukamba Amesema kuwa jambo kubwa ambalo watoto wanatakiwa kurithi kutoka kwa wazazo wao ni Elimu hivyo wazazi wametakiwa kulipa kipaumbele suala la elimu ili kuleta maendeleo katika jamiiAidha Mhe. Serukamba ameongeza kwa kuwataka wasomi wote kujijengea tabia ya kujifunza kila siku kwa kusoma vitabu mbalimbali kwani kwa sasa sayansi na teknolojia ikekuwa kwa kasi tofauti na hapo awali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.