Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa onyo kali kwa wauzaji wa dawa kiholela akisema kuwa Serikali haitamfumbia macho mtu yoyote atakae kutwa na dawa bandia.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutanisha waandishi wa habari na wahariri wa habari kuhusu utekelezaji wa Dawa na Vifaa Tiba kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sun Set Hotel kilichoandaliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).
Akifungua kikao hicho Mhe. Serukamba amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la watu kujiuzia dawa kiholela Serikali imejipanga kuhakikisha inatokomeza wauzaji wa dawa kiholela na kuwachukulia hatua kali pindi watakapobainika
Pia ameongeza kwa kuwataka waandishi wa habari kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili kuepukana na kununua dawa zinazouzwa mikononi na baadhi ya watu.
Kikao hicho kimewakutanisha washiriki toka Mkoa wa Singida,Dar es salaam, Dodoma na Iringa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.