Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego amewataka wananchi wanaoishi Mkoa wa Iringa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha Mvua kwa kuhakikisha wanalinda Afya zao
Mhe. Dendego ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa katika kipindi hiki ambacho kumeripotiwa kuwa na mvua kubwa wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa wazazi kuhakikisha wanakuwa jirani sana watoto wao pia kuchukua tahadhari za kiafya kwani uwepo wa mvua unapelekea kutokea kwa magonjwa mbalimbali ya mlipuko pia ameongeza kwa kusema kuwa kwa wananchi wote waliopo maeneo ya mabondeni ambayo ni hatarishi wanapaswa kuhama mara moja kuepuka majanga ya mvua hizo.
Aidha Dendego amewataka viongozi wa kila Halmashauri wanatoa elimu kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na makanisani kuhusu uwepo wa mvua hizi kubwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.