Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewataka viongozi wa machinga kwa Umoja wa Machinga SHIUMA na wale wa Iringa Machinga Network kukaa meza moja na kumaliza tofauti zilizopo ili kuwaweka pamoja machinga hao na kuepukana na makundi yaliyopo kwasasa.
Akizungumza na machinga wakati alipokutana nao kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo Mhe. Dendego baada ya kusikiliza pande zote mbili amewaomba viongozi hao kukaa kwa pamoja kuzungumza kwa nia njema ili kuwaunganisha machinga hawa waweze kufanya kazi na kujipatia kipato.
Pia Mhe. Dendego ameendelea kuwahimiza machinga hao kufanya kazi kwa bidiii kuacha kulalamika kwenye mitandao na badala yake wafike katika Ofisi za Serikali kuweza kuonana na viongozi kuwaelezea shida zao.
Nae kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amewataka machinga hao kutumia vyema mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwaingizia kipato na si kutumia mitandao hiyo kuleta migogoro kwenye jamii
Kikao hicho kimewahusisha viongozi wa Bodaboda,Bajaj,Daladala na Machinga wa Soko la Mlandege
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.