Vyama vya ushirika katika mikoa ya nyanda za juu kusini vimetakiwa kushikamana katika kukuza ushirikiano na mtaji.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipotembelea banda la Manispaa ya Iringa katika maonesho ya Nanenane katika uwanja wa John Mwakangale mjini Mbeya.
Masenza alisema kuwa wanaushirika wanatakiwa kushikamana ili kuimarisha umoja na kukuza mtaji wao. “Wanaushirika mnapopotezana, ushirika unaparaganyika. Wanaushirika tushikamane ili kudumisha ushirika hasa kina mama” alisema Masenza.
Masenza alisema kuwa vijana wamekuwa wagumu kujiunga na vyama vya ushirika na kuwaacha watu wazima na wazee katika sekta ya ushirika. Aliwataka wanaushirika kubuni mbinu za kuwavutia vijana ili wajiunge na ushirika.
Wakati huohuo, mkuu wa mkoa aliwasisitiza wakina mama kuonesha ushupavu katika ushirika kusimamia na kuimarisha ushirika. Aliwashauri wakina mama kuanzisha tawi B katika ushirika kwa ajili ya watoto wao ili kuwarithisha dhana ya ushirika.
Maonesho ya shughuli za wakalima Nanenane mwaka 2017 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi kufikia uchumi wa kati”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.