Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima O. Dendego amewataka Wakuu wa Wilaya na Viongozi wengine kuhakikisha wanasimamia vyema na kufanya ukaguzi wa Miradi ya Barabara ili kubaini dosari zilizopo katika Barabara hizo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Mhe. Dendego amesema kuwa serikali inatumia fedha nyingi katika matengenezo ya barabara hivyo viongozi wanatakiwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuzikagua barabara hizo.
"Ninapenda kutumia nafasi hii kuwataka Wakuu wa Wilaya wakurugenzi kukagua mara kwa mara utekelezaji wa miradi ya barabara na kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika wanapobaini kuwepo kwa dosari au kukiukwa kwa taratibu wakati wa matengenezo au ukarabati wa Barabara"
Aidha Mhe.Dendego ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo ya hifadhi za barabara hususani katika kipindi cha mvua.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.