Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ameendelea na ziara ya kukagua miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na kupongeza baadhi ya miradi.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe. Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kutoa fedha kiasi cha Shilingi Millioni 30 ya kukamilisha ujenzi wa hostel ya shule ya wasichana iliyopo katika kata ya Itandula iliyojengwa kwa mapato ya ndani ambapo mpaka sasa ujenzi umegharimu zaidi ya shilingi Millioni mia tatu.
Pia Mhe. Serukamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupeleka mifuko Ishirini ya Saruji katika shule ya Msingi Mtambula ili kukamilisha Ofisi ya walimu.
Sambamba na hayo Mhe. Serukamba amemtaka Mhandisi wa Halmashauri hiyo kutokukaa Ofisini na badala yake ahakikishe anatembelea miradi yote na kuikagua kujua imefikia wapi.
Kwa upande mwingine baadhi ya wananchi wametoa shukrani nyingi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi anazozitoa kwaajili ya kuwajengea shule na vituo vya afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Anuani ya Posta: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Simu: +255 262 702 715
Mobile:
Barua pepe: ras@iringa.go.tz
Hakimiliki ©2024, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.