Mkoa wa Iringa una Halmashauri Tano (5) ambazo ni Halmashauri ya Manispaa Iringa, Iringa DC, Kilolo DC, Mafinga TC na Mufindi DC.
Halmashauri za Wilaya zinaongozwa na Wenyeviti na Halmashauri ya Jiji inaongozwa na Mstahiki Meya ambao ni Wenyeviti wa Halmashauri, kwa kushirikiana na Wakurugenzi ambao ni Watendaji wakuu wa Halmashauri husika .
Halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Iringa hutoa huduma za Kiuchumi zikiwepo kilimo, mifugo, misitu, Uvuvi, Miundombinu, huduma za jamii kama afya, maji, elimu, maeneo ya burudani, mazishi, mipango miji, kutunza mazingira, ustawi wa jamii, ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla.
Utawala Bora
Utawala bora ni suala linalotekelezwa na Halmashauri zote katika nyanja za:
• Demokrasia
• Ushirikishwaji
• Utawala wa sheria
• Uadilifuwa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
• Uwazi na Uwajibikaji
• Ufanisi katika utendaji kazi
• Mchakato wa kijinsia
• Upangaji mipango
• Ujuziwa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo
• Utekelezajiwa Mipango.
MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.
Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa nasheria hiyo ni kama ifuatavyo:-
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.