Dkt. MGIMBA AONGOZA TIMU KUKAGUA MIUNDOMBINU YA AFYA IRINGA
Timu ya Afya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa ikiongozwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Credinus Mgimba, imefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya afya Ndani ya siku tatu katika Halmashauri za Mkoa wa Iringa. Lengo la ukaguzi huo ni kuhakikisha fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya afya zinatumika ipasavyo na miradi inakamilika kwa wakati.
Ukaguzi huo umejikita katika ujenzi wa vyoo, vichomea taka, pamoja na ukarabati wa vyumba vya kujifungulia (labor ward) na miundombinu mingine ya Zahanati, kati ya zahanati zilizotembelewa ni Zahanati ya Lusinga iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Kilolo yenye ujenzi unaogharimu Shilingi Millioni 58.8 na Zahanati ya Irole yenye mradi wa Ujenzi unaogharimu Shilingi Millioni 59.8 Hata hivyo hali ya ukarabati inaendelea vizuri, ambapo baadhi ya zahanati tayari zimekamilisha utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, Dkt. Mgimba amewataka viongozi wa afya wa halmashauri pamoja na viongozi wa kijiji kuendelea kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili kuhakikisha inakidhi viwango vinavyohitajika na kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.