TAARIFA YA KUWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA MABANDA YA MKOA WA IRINGA KATIKA MAONESHO YA NANENANE 2025
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James, anayofuraha, kuwakaribisha wananchi wote kushiriki na kutembelea mabanda yetu katika Maonesho ya Kilimo na Mifugo ya Nanenane yanayofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025 katika Viwanja vya John Mwakangale – Jijini Mbeya.
Katika maonesho haya, Mkoa wa Iringa utakuwa ukionesha mafanikio mbalimbali ya sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu, viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, teknolojia bunifu, pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri, Taasisi na wadau wa maendeleo kutoka mkoani kwetu.
Wananchi watapata nafasi ya:
●Kujifunza mbinu bora za kilimo cha kisasa na mifugo
●Kupata ushauri kutoka kwa wataalam wa sekta mbalimbali
●Kufahamu fursa za uwekezaji na biashara zilizopo ndani ya Mkoa wa Iringa
●Kujionea bidhaa bora zinazozalishwa na wakulima na wajasiriamali wa mkoa wetu
Tunawaalika kwa moyo mkunjufu kutembelea mabanda yetu na kushiriki kikamilifu katika maonesho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 4 Barabara ya Pawaga
Postal Address: P.O.Box 858, 51108 Gangilonga, Iringa, Tanzania
Telephone: +255 262 702 715
Mobile:
Email: ras@iringa.go.tz
Copyright ©2024 Iringa Regional Secretariat. All rights reserved.